Kuhusu Ufunuo Huu

Huu ni ufunuo wa Yesu Kristo aliopewa na Mungu ili apate kuwaonyesha watumishi wake mambo yatakayotokea karibuni. Kristo alimtuma malaika wake amjulishe mtumishi wake Yohana, ambaye ameandika yale yote aliyoyaona, yaani ujumbe wa neno la Mungu na ushuhuda wa Yesu Kristo. Amebarikiwa anayesoma maneno ya unabii huu na wale wanaosikiliza na kuzingatia yale yaliyoandikwa humu, maana wakati umekaribia.

Salamu Kwa Makanisa Saba

Kutoka kwa Yohana. Kwa Makanisa saba yaliyoko Asia: Ninawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu aliyeko, ambaye alikuwako na atakayekuja; na kutoka kwa wale roho saba walioko mbele ya kiti chake cha enzi;

na kutoka kwa Yesu Kristo ambaye ni shahidi mwaminifu, wa kwanza kufufuliwa kutoka kwa wafu, na ambaye ni mtawala wa wafalme wa dunia. Yeye anatupenda na ametuweka huru kutoka katika dhambi zetu kwa damu yake;

akatufanya sisi kuwa wafalme na makuhani, tum tumikie Mungu Baba yake. Utukufu na uwezo ni wake milele na milele! Amina.

Tazama! Anakuja katika mawingu! Na kila jicho litamwona. Hata na wale waliomchoma mkuki na makabila yote ulimwenguni wataomboleza kwa ajili yake. Naam. Amina. “Mimi ni Alfa na Omega,” asema Bwana Mungu, “Aliyeko na aliyekuwako na ata kayekuja, Mwenyezi.”

Yohana Alivyopata Ufunuo

Mimi ni Yohana, ndugu yenu na mwenzenu katika mateso, na katika ufalme na subira kwa ajili ya Yesu Kristo. Niliwekwa katika kisiwa cha Patmo kwa ajili ya kutangaza neno la Mungu na kumshuhudia Yesu. 10 Basi, siku ya Bwana nilikuwa katika Roho, nikasikia sauti kubwa kama ya tarumbeta nyuma yangu 11 ikasema, “Andika haya yote unayoyaona kwenye kitabu, kisha ukipeleke kwe nye makanisa saba yafuatayo: Efeso, Smirna, Pergamo, Thiatira, Sardi, Filadelfia na Laodikia.”

Sardi, Filadelfia na Laodikia.”

12 Ndipo nikageuka ili nione ni sauti ya nani iliyokuwa ikisema nami. Na nilipogeuka, nikaona vinara saba vya taa vya dhahabu. 13 Katikati ya vile vinara, nikaona mtu kama mwana wa Adamu, amevaa kanzu ndefu na mkanda wa dhahabu kifuani. 14 Kichwa chake na nywele zake zilikuwa nyeupe kama sufu, nyeupe kama theluji; na macho yake yalikuwa kama moto uwakao. 15 Miguu yake ilikuwa kama shaba iliyosuguliwa sana, kama vile imesafishwa katika tanuru ya moto; na sauti yake ilikuwa kama sauti ya mapo romoko ya maji. 16 Katika mkono wake wa kulia alishika nyota saba, na kinywani mwake mlitoka upanga wenye makali kuwili. Uso wake uling’aa kama jua kali.

17 Nilipomwona, nilianguka miguuni pake kama mfu. Lakini yeye akaweka mkono wake wa kulia juu yangu akasema, “Usiogope. Mimi ni wa kwanza na wa mwisho. 18 Mimi ni Yeye aliye hai; nili kufa na tazama, mimi ni hai milele na milele! Nami ninazo funguo za mauti na kuzimu. 19 Basi andika mambo uliyoyaona, yaliyopo na yatakayotokea baadaye. 20 Maana ya zile nyota saba ulizoziona katika mkono wangu wa kulia na vile vinara saba vya taa vya dha habu ni hii: zile nyota saba ni malaika wa yale makanisa saba; na vile vinara saba ni hayo makanisa saba.”